Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko amejiunga na kinyang’anyiro cha kuwania kiti cha ugavana Mombasa.
Wiper Democratic Movement iliwasilisha jina la Sonko kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuwa miongoni mwa walioidhinishwa kushiriki uchaguzi wa mchujo wa chama.

Bosi huyo wa zamani wa Kaunti ya Nairobi atachuana vikali na Mbunge wa Kisauni Ali Mbogo, ambaye pia anawania tiketi ya Wiper.
Mshindi atachuana na aliyekuwa Seneta wa Mombasa Hassan Omar, ambaye amepewa tikiti ya moja kwa moja ya UDA.

Tikiti ya ODM ni vita kati ya Mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharif Nassir na bilionea wa Mombasa Suleiman Shabal.
Sonko alikaribishwa rasmi kwa Wiper na kiongozi wa chama Kalonzo Musyoka mnamo Machi 25, huku timu yake ikidokeza kwamba anazingatia mipango ya kutwaa tena kiti chake kama mkuu wa Kaunti ya Nairobi.
How goes it, great webpage you’ve got in here. lialda à commander en ligne en Suisse